27 Sep Mkate Murua wa Zabibu Kavu

MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA
saa 2

UGUMU


KWA
Watu 4
1
Weka unga, hamira, sukari na chumvi kwenye bakuli kisha vichanganye vikiwa vikavu.
2
Ongeza yai, siagi, na maji; kanda mpaka manda iache kuganda mkononi.
3
Funika na utandao wa plastiki (cling film) au kitambaa kisafi kisha acha manda itulie kwa muda wa dakika 10 kwenye sehemu ya baridi.
4
Toa hewa kisha igawe kwenye vipande vya gramu 130 na viunde viwe mviringo kisha viweke kwenye sehemu ya baridi kwa muda wa dakika 20.
5
Sukuma kila kipande kwenye kibao. Weka vipande 3 kimoja juu ya kingine ukinyunizia unga wa maizena kabla ya kulundika.
Sukuma kila fungu la vipande vitatu vitatu na mpini wa kusukumia.
6
Paka jemu ya aprikoti kwenye miviringo mikubwa iliyoundwa kwa kusukuma pamoja miviringo mitatu.
7
Sambaza zabibu kavu na kunja kwa kuzungusha iwe kama mpini. Kata slesi upate vipande vya mviringo vyenye upana wa takriban sentimita 2.
8
Vipange vimviringo hivyo kwenye sinia ya oveni.
9
Acha viumuke kwa muda wa saa 1.
10
Paka vya kupambia juu kisha oka kwenye oveni yenye joto la 200°C kwa muda wa dakika 18.
Mbinu: Tumia maizena kufanya iwe na mwonekano wa kuchambuka, kama kwason (mkate wa Kifaransa uliotengenezwa wa siagi unaochambuka).
You may also like:
Sorry, the comment form is closed at this time.