Hambaga ya Kukaanga

Hambaga ya Kukaanga

preparation-75x75

MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA

Saa 2

difficulty-75x75

UGUMU

easy
portions-75x75

KWA

Watu 4

Whisk

VIAMBATO

 • 250g za unga
 • 150ml za maji ya vuguvugu
 • Kijiko kidogo 1 cha chumvi
 • 5 1/2g za hamira ya Saf-Instant
 • 30g za siagi laini
 • 150g za nyama ya kusaga iliyoundwa kama bapa la mviringo x 4
 • Nyanya 1 iliyosagwa
 • Nyanya 1 iliyokatwa slesi
 • Slesi nne za vipande vya jibini laini
 • Majani manne ya saladi
 • Kijiko kikubwa 1 cha kitimiri
 • Kitunguu 1 kilichosagwa
 • Vipande 3 vya kitungu saumu
 • Kijiko kidogo 1 cha pilipili manga
 • Kijiko kidogo 1 cha unga wa nyanya
 • Mafuta ya kukaangia

BIDHAA INAYOANGAZIWA

SAF-INSTANT-11g-RED

1

Weka unga, chumvi, unga wa nyanya na hamira ya Saf-Instant kwenye bakuli kisha changanya.

2

Tengeneza tundu katikati, ongeza maji na siagi laini alafu kanda na unda manda iwe kama mpira.

3

Funika na acha itulie kwa muda wa saa 1.

4

Toa hewa kwenye manda, kanda alafu gawa kwenye vipande vinne na viunde viwe mviringo.

5

Kandamiza kila mviringo kisha acha viumuke kwa muda wa saa 1.

6

Kaanga kwa muda wa dakika 3 hadi 4 kwenye mafuta ya moto wa wastani, kisha toa ukaushe kwenye karatasi ya kunyonya mafuta.

7

Kwa vijazio: Katika kikaangio weka mafuta, vibapa vya nyama, chumvi, pilipili manga, kitunguu, nyanya ya kusagwa, kitunguu saumu na kitimiri. Changanya na pika kwa muda wa dakika 5.

8

Yayusha vipande vya jibini.

9

Pangilia hambaga.

You may also like:

No Comments

Sorry, the comment form is closed at this time.