21 Jul Mkate wa Pilipili Manga
MUDA
Saa 2:45
UGUMU
KUTOSHA
Watu 4
1
Weka unga, chumvi, hamira, pilipili manga nyeupe, maziwa na sukari kwenye bakuli kisha vichanganye vikiwa bado vikavu.
2
Ongeza maji na mafuta ya kupikia; kanda mpaka manda iache kuganda mikononi.
3
Acha itulie kwenye bakuli kwa muda wa dakika 30.
4
Kanda tena kidogo kuondoa hewa kisha gawanya kwenye vipande vya takriban gramu 90-100, alafu weka kwenye vyombo vya kuokea.
5
Acha viumuke kwa muda wa saa 1 na dakika 40.
6
Oka kwenye oveni yenye joto la 200oC kwa muda wa dakika 18.
You may also like:
Sorry, the comment form is closed at this time.