04 Jul Pizza ya Zaatar
MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA
Saa 1h50
UGUMU
KWA
Watu 4
1
Mimina maji ya vuguvugu kisha koroga hamira ya Saf-instant® kwenye bakuli kubwa.
2
Weka unga, chumvi na mafuta ya zaituni Changanya mpaka manda ichanganyike vizuri.
3
Kanda kwa muda wa dakika 5.
4
Unda manda kwenye mviringo kama mpira, funika kisha acha iumuke kwa muda wa saa 1.
5
Baada ya manda kuumuka vizuri, igawanye kwenye vipande 4 vilivyo sawa.
6
Tengeneza vipande viwe miviringo kama mpira kisha acha vitulie kwa muda wa dakika 10.
7
Tayarisha vijazio kwa kuchanganya zaatar na mafuta ya zaituni.
8
Chukua mipira ya manda ikandamize iwe tambarare alafu weka vijazio.
9
Oka kwenye oveni iliyopashwa moto hadi mionzi ya 240°C kwa muda wa dakika 15.
Unaweza pia kupenda:
Sorry, the comment form is closed at this time.