22 Apr Vitumbua vya nazi
MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA
1h20
UGUMU
KWA
Watu 2
VIAMBATO
- 5.5 g hamira ya Saf-instant Dry Yeast
- 300g mchele mweupe
- 50 g za unga
- 250 ml tui la nazi la kopo lililopashwa moto
- 3 vijiko vidogo vya machicha ya nazi yaliyokaushwa
- 1 kijiko kidogo cha chumvi
- 100g sukari ya kahawia
- 1 kijiko kidogo cha iliki
- 1 kijiko kidogo cha kungumanga iliyosagwa
- 1/2 tsp kidogo cha uto wa lozi
BIDHAA INAYOANGAZIWA
1
Anza na kuloweka mchele kwenye bakuli kubwa na acha ulainike kwa muda wa saa 12.
2
Baada ya kuuloweka, utoe maji kabisa. Katika mashine ya kusagia viambato (blenda) changanya tui la nazi, machicha ya nazi, iliki, kungumanga, uto wa lozi, sukari, chumvi na hamira ya Saf-instant Dry Yeast.
3
Changanya mpaka vilainike na viwe kama malai. Mimina mchanganyiko kwenye bakuli kisha ufunike na uache uumuke kwenye sehemu yenye joto kwa muda wa saa moja.
4
Pasha mafuta moto kwenye kikaangio kwenye jiko lenye moto wa wastani.
5
Kikaangio kikishapata moto, mimina mchanganyiko kwenye kila tundu la kikaangio, upawa mmoja mmoja. Kaanga kila upande kwa muda wa dakika 2 hadi 3, mapaka viwe na rangi ya kahawia.
6
Baada ya kuvikaanga, viweke kwenye tishu ya jikoni kukausha mafuta.
Burudika na vitumbua vyako ulivyopikia nyumbani!
You may also like:
Sorry, the comment form is closed at this time.