27 Sep Galeti ya Chungwa
MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA
saa 2
UGUMU
KWA
Watu 6
1
Weka unga, chumvi, sukari na hamira kwenye bakuli; vichanganye vikiwa vikavu.
2
Ongeza yai, mafuta, maziwa, uto wa chungwa na maji ya machungwa. Kanda mpaka upate manda iliyochanganyika vizuri. Ongeza gamba la chungwa lililokwaruzwa na endelea kukanda mpaka manda iache kuganda mikononi.
3
Unda iwe kama mpira na iache itulie kwenye bakuli kwa muda wa dakika 10.
4
Toa hewa na isukume na mpini wa kusukumia iwe tambarare yenye unene wa milimita 5 kisha ikate vipande na bati la kukatia biskuti. Viweke kwenye sinia.
5
Acha viumuke mahali penye joto la kawaida kwa muda wa saa 1.30.
6
Kaanga kwenye mafuta ya moto.
You may also like:
Sorry, the comment form is closed at this time.