Mafini ya Mkate Mtamu yenye Chokoleti na Karanga

Mafini ya Mkate Mtamu yenye Chokoleti na Karanga

preparation-75x75

MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA

Saa 2

difficulty-75x75

UGUMU

easy
portions-75x75

KWA

Watu 6

Whisk

VIAMBATO

  • 450g za unga
  • 70g za sukari
  • Kijiko kidogo 1 cha chumvi
  • 5 1/2g za hamira ya Saf-Instant
  • Mayai 2 na yai 1 la kupambia
  • Kijiko kikubwa 1 cha siagi laini
  • 125ml za maziwa ya vuguvugu
  • 50g za chokoleti iliyo katwa vipande vidogo vidogo
  • 30g za karanga zilizopondwa pondwa

BIDHAA INAYOANGAZIWA

SAF-INSTANT-11g-RED

1

Weka unga, chumvi, sukari, karanga na hamira kwenye bakuli kisha vichanganye vikiwa vikavu.

2

Ongeza mayai, maziwa, siagi alafu changanya vyote.

3

Kanda mpaka manda iache kuganda mikononi. Unda iwe mviringo kama mpira, funika na iache iumuke kwa muda wa saa 1.

4

Toa hewa kwenye manda na ikate vipande 6.

5

Viunde viwe kama mpira kisha viweke kwenye chombo cha kuokea mafini.

6

Funika na viache viumuke kwa muda wa dakika 30.

7

Vipange kwenye chombo kikubwa zaidi ukiacha nafasi ya kutosha kati ya kila moja, paka yai lililopigwa juu alafu nyunyizia vipande vya chokoleti.

8

Oka kwenye oveni yenye joto la 180oC kwa muda wa 20 min.

You may also like:

No Comments

Sorry, the comment form is closed at this time.