05 Nov Mkate Sukari wa Nazi


MUDA
Saa 2:30

UGUMU


KUTOSHA
8 persons
1
Weka maji ya vugu vugu na tui la nazi ndani ya bakuli la kuchanganyia na changanyia humo hamira.
2
Ongeza unga, chumvi, sukari, machicha ya nazi, na siagi au majarini. Changanya manda mpaka yote itakapo kuwa inaugumu sawa.
3
Kanda kwa dakika 5.
4
Unda manda iwe kwenye umbo la mpira. Acha itulie kwa muda wa dakika 45
5
Unga ukishaumuka, gawa kwenye vipande 2 vinavyolingana
6
Viunde viwe na umbo la mviringo. Acha vitulie kwa muda wa dakika 15
7
Sasa unda vipande kwenye umbo la boflo la mkate. Viviringishe kwenye machicha ya nazi kisha viweke kwenye bati la mkate.
8
Acha vitulie kwa muda wa saa 1.
9
Paka kuu yai lililopigwa. Chanja chanja juu ya mkate. Oka kwenye oveni iliyokwisha pashwa moto hadi 190°C kwa muda wa dakika 20.
You may also like:
Sorry, the comment form is closed at this time.