07 Jul Mkate wa kukaanga kwa kuku
MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA
Saa 2h30
UGUMU
KWA
Watu 4
VIAMBATO
- 5.5g za hamira ya Saf-Instant
- 425g za unga
- 1 kijiko kidogo cha chumvi
- 2 kijiko kidogo cha sukari ya kahawia
- 250 ml za maji ya vuguvugu
- 1/2 kijiko kidogo cha iliki
- 2 vijiko vikubwa vya mafuta
- 1 kijiko kidogo cha pilipili manga
- 1 kijiko kidogo cha tangawizi iliyosagwa
- Chumvi kidogo
- 1 karoti
- 1 kitunguu chekundu
- 1 pilipili hoho
- 250 g za minofu ya kuku
- 3 vipande vya kitunguu saumu
BIDHAA INAYOANGAZIWA
1
Weka unga, chumvi, sukari, iliki na hamira ya Saf-Instant kwenye bakuli kisha vichanganye na tengeneza tundu katikati.
2
Mimina maji ya vuguvugu kwenye tundu kisha kanda manda mpaka ichanganyike vizuri.
3
Funika na kitambaa kisafi kisha acha iumuke kwenye sehemu yenye joto la wastani kwa muda wa saa 1.
4
Kanda manda tena mpaka iwe imara zaidi. Sukuma manda mpaka iwe na unene wa 2 cm kisha kata miviringo kadhaa. Acha iumuke kwa muda wa saa 1.
5
Kaanga miviringo kwenye mafuta mengi mpaka igeuke rangi ya kahawia isiyokolea sana. Baada ya kuiva, itoe kwenye mafuta na iweke kwenye karatasi ya jikoni iyonye mafuta.
6
Acha ipoe kisha kata kila kipande katikati ili kuweka vijazio vya kuku.
7
Weka mafuta kwenye sufuria na kaanga kitunguu na vitunguu saumu vilivyo katwa katwa. Ongeza minofu ya nyama ya kuku na tangawizi iliyosagwa.
8
Weka, chumvi na pilipili manga kisha pika kwa muda wa dakika 5. Ongeza pilipili hoho na karoti kisha endelea kupika kwa muda wa dakika 5 zaidi.
9
Jazia kijazio cha nyama ya kuku.
10
Huu Tayari!
Unaweza pia kupenda:
Sorry, the comment form is closed at this time.