Pai Ndogo za Matufaa na Karanga

Pai Ndogo za Matufaa na Karanga

preparation-75x75

MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA

saa 1

difficulty-75x75

UGUMU

easy
portions-75x75

KWA

Watu 6

Whisk

INGREDIENTS

 • gramu 500 za unga
 • gramu 100 za maji
 • gramu 10 za chumvi
 • Matufaa (apple) 3
 • gramu 6 za hamira ya Saf-Instant
 • Mayai 2
 • gramu 50 za siagi
 • gramu 100 za maziwa
 • gramu 30 za sukari
 • gramu 200 za jemu ya aprikoti
 • gramu 100 za karanga zilizopondwa

BIDHAA INAYOANGAZIWA

SAF-INSTANT-11g-RED

1

Weka unga, chumvi, sukari na hamira kwenye bakuli, kisha vichanganye.

2

Ongeza yai, maziwa, siagi na maji, alafu changanya vyote.

3

Kanda mpaka manda iache kuganda mikononi. Umba mpira wa manda kisha acha itulie kwa muda wa dakika 10.

4

Gawanya kwenye vipande vya takriban gramu 50 na acha vitulie wa muda wa dakika 5.

5

Sukuma vipande hivyo kwa utumia mpini na viweke kwenye vyombo ya kuokea vilivyopakwa mafuta kidogo.

6

Ndani, panga matufaa yaliyokatwa kama slesi na kisha weka jemu.

7

Oka kwenye oveni yenye joto la 200oC kwa muda wa dakika 15.

8

Vikiisha iva, nyunyizia karanga zilizopondwa pondwa.

You may also like:

No Comments

Sorry, the comment form is closed at this time.